skip to Main Content

picha na mtandao

KATAVI

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni kuhusiana na maboresho ya barabara yanayoendelea kufanywa na TARURA

Wakizungumza na Mpanda radio FM wamesema kuwa maboresho hayo  ya Barabara yakamilishwe kwa wakati

Kwa upande wake meneja wa TARURA Injinia Kahoza Joseph amebainisha kuwa matengenezo hayo yanafanyika kupitia  fedha za mpango wa matengenezo ya barabara za tozo  za mwaka 2023/2024.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu inayoboreshwa kwa kuacha kutupa takataka kwenye mitaro, makaravati  kwani gharama zinazotumika ni kubwa .

Back To Top