skip to Main Content

MPANDA

Kamati za shule za msingi katika halmashuri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi zimetakiwa kuhakikisha zinafuatilia miradi inayofanyika katika shule za msingi.

Hayo yamezungumzwa na kaimu afsa elimu msingi wa halmashuri ya manispaa ya Mpanda Victor Mwakajumlwa katika semina ya mafunzo iliyohusisha kamati za shule za msingi ambapo amesema ni jukumu la kamati na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanasimamia miradi yote inakwenda kwa mujibu wa taratibu wa sheria na fedha zote zilizotolewa na serikali hazipotei

Kwa upande wake kaimu afsa manunuzi halmashuri ya manispaa mwalimu Kiloba Ahamad amewaomba wananchi na kamati za shule za msingi kufuatilia matumizi yote ya vifaa yanayofanyika katika miradi inayotekelezwa katika shule husika

Kwa upande wao washiriki wa semina ambao wanaunda kamati za shule za msingi katika halmashuri ya manispaa ya Mpanda wamesema kuwa kupitia Mafunzo yamewasaidia kuweza kufahamu ni namna gani wanakwenda kufuatilia na kusamimia miradi hiyo huku wakiahidi kwenda kuelimisha jamii

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania DR Samia Suluhu Hassani kutoa zaidi ya shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mpya za msingi na madarasa katika halmashuri ya manispaa ya Mpanda.

Back To Top