skip to Main Content

MPANDA

Zaidi ya wanafunzi  5000 katika  Kata ya Shanwe manispaa ya Mpanda mkoani katavi  hawana sehemu ya  kusomea hali ambayo inapelekea kusomea nje.

Akizungumza na Mpanda Redio FM Diwani wa Kata ya Shanwe Masumbuko Makolo kolo amesema kuwa shule zilizopo katika  kata hiyo  zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa zaidi ya 100, madawati na walimu

.

Aidha Makolo kolo amesema kuwa licha ya jitihada za serikali na wananchi kuendelea kunusuru changamoto hizo ameiomba serikali kuongeza jitihada zaidi katika kutatua chanamoto hiyo na sio kuwaachia mzigo mkubwa wananchi.

.

Kwa mujibu wa makolokolo changamoto za miundo mbinu hupelekea   kushuka kwa ufaulu na  kuongezeka kwa watoto wa mitaani .

Back To Top