skip to Main Content

MPANDA

Wazazi na Walezi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuwapa kipaumbele watoto katika kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.

Akizungumza katika hafla ya kutunukiwa udaktari kutoka chuo cha all nation christian church Askofu Laban Ndimubenya amewataka wazazi na walezi kuona umuhimu wa elimu kwa watoto wao kwani huo ni urithi pekee ambao mtoto anaweza kunufaika nao.

Aidha kwa upande wake Mke wa askofu huyo amepongeza jitihada zilizofanywa hadi kutunukiwa udaktari huo huku akiwataka wazazi na walezi kuendelea kusimamia katika misingi ya kuhakikisha mtoto anapata elimu.

Back To Top