skip to Main Content

MPANDA

Jeshi la polisi mkoa wa katavi limefanikiwa kuwakamata watu watano wakiwa na kilo nne na kete mia mbili na tisa za madawa ya kulevya aina ya bangi.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi ACP Ally Makame Hamad amesema kuwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo wamefanikiwa kuwakamata watu watano wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya aina ya bangi na tayari kesi yao imefikishwa mahakamani.

Sambamba na hilo jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kuwakamata watu wawili Omary Lukele miaka 56 na Denis Davis miaka 44 wakiwa na meno ya tembo vipande sita ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa kwenye mfuko wa salufeti na kufichwa ndani ya nyumba wanayoishi.

Kamanda makame amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia doria na msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi kuanzia mwezi wa pili hadi wa tatu mwaka huu.

Back To Top