skip to Main Content

KATAVI
Watu watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa Mkoani Katavi mara baada ya kukutwa na hatia ya mauaji katika matukio mawili tofauti .

Jeshi la polisi Mkoa wa katavi Limesema limepata mafanikio mahakamani kutokana na kesi za watuhumiwa wa makosa ya mauaji ambao wamekutwa na hatia na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa sheria .

Akitoa taarifa hiyo kamanda wa Polisi Mkoa wa katavi Ally Makame Hamad amesema mahakama kuu imewakuta na hatia ya mauaji watu hao kutoa hukumu hiyo.

Aidha katika tukio lingine jeshi la polisi mkoa wa katavi linamtafuta Michael Msapi mkazi wa kirando mkoa wa Rukwa kwa kosa la kumng’ata mama yake masikio yote mawili kwa tuhuma za imani za kishirikina.

Jeshi la polisi mkoa wa katavi linawahimiza wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu ili kuendelea kuufanya mkoa kuwa salama

Back To Top