Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Tank za maji zikiwa chini na wameeleza tank hizo ni Mbovu.picha na Rahel Ezekia
KATAVI
Baadhi ya madereva wa usafirishaji abiria wa stand ya zamani pamoja na wafanyabiashara waliopo katika eneo hilo manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuboresha miundombinu ya eneo hilo ikiwemo choo na maji.
Wameyasema hayo katika mahojiano na Mpanda Redio fm wamebainisha kuwa miundombinu ya stendi hiyo inaharibu baadhi ya magari licha ya kuwa wanatoa ushuru bado serikali haifanyi ukarabati kwa wakati
Kwa upande wake Jofrey Sigulu mwenyekiti wa eneo hilo amebainisha kuwa amekuwa akifanya jitihada mbalimbali za kufikisha taarifa kwa mkurugenzi kuhusu miundominu ya stendi hiyo pamoja na ukarabati wa choo ambao unaathiri utendaji kazi wa wafanyabiashara wa eneo hilo
Nae Festo Tayari katibu wa stendi ya zamani ameiomba serikali kupitia ushuru ambao wanatoa utumike kufanya marekebisho katika eneo hilo huku wakimuomba mkurugenzi kufika katika eneo hilo ili aone hali ya miundombinu ilivyo mibovu.
Mpanda Redio fm inaendelea na jitihada ili kuzungumza na mkurugenzi mtendaji manispaa ya Mpanda aweze kutolea majibu ya changamoto hiyo