skip to Main Content

KATAVI

Wananchi ambao bado hawajachangia katika ujenzi wa Shule mpya ya Msasani kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameombwa kuchangia ili kuikamilisha shule hiyo.

Wakizungumza na Mpanda Radio Baadhi ya Wananchi waliochangia Ujenzi wa Shule hiyo wamewaomba wananchi kuendelea kutoa mchango ili kuwaondolea adha watoto wanaorundikana katika shule za Jirani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya mapokezi ya Vifaa katika ujenzi wa shule ya Msingi Msasani Deus Juvenali amewaomba Wadau na Wananchi kusaidia ukamilishwaji wa Ujenzi wa Boma la Vyumba Viwili na Ofisi vya Shule ya Msingi Msasani.

Back To Top