Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Wananchi Manispaa ya Mpanda wamelalamikia baadhi madereva wa vyombo vya moto mkoani hapa kutozingatia sheria za usalama barabarani hali inayopelea ajali zisizo na ulazima.
Wakizungumza na Mpanda Radio fm wameeleza changamoto wanayoipata kutokana na madereva kushindwa kuzingatia sheria za usalama wa barabarani ni kutokea kwa ajali hasa kwa watembea kwa miguu.
Aidha kwa upande wa madereva mkoani hapa wamekiri uwepo wa madereva ambao hawazingatii sheria za usalama wa barabarani ikiwemo kuendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kitengo cha usalama barabarani Geofrey Brighton amewataka madereva kuzingatia Sheria zilizopo na wanaokiuka wakibainika adhabu huchukuliwa dhidi yao ikiwemo kutozwa faini na kupelekwa Mahakamani.
Katika hatua nyingine Brighton ametoa ushauri kwa madereva kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani pamoja na watembea kwa miguu kuchukua tahadhari