miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
KATAVI
Wananchi mkoani Katavi wamepaswa kufichua na kushiriki katika kutoa taarifa na vitendo vya kiharifu ili kukomesha vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na Inspekta Kelvin Fuime kutoka ofisi ya kamanda wa polisi mkoa dawati la jinsia, ambapo amesema ni wajibu wa mwananchi kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la polisi katika kuripoti taarifa zote zinazoashiria uvunjivu wa amani na upotevu wa mali za jamii.
.
Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa kushirikishwa katika kutoa ushahidi na kuhofia usalama wa maisha yao baada ya kuwafichua waharifu hali inayopelekea kutotoa taarifa hizo.
.
Aidha Inspekta Kelvin Fuime amewaasa wananchi kuwa ni muhimu kuripoti taarifa zanye uhakika ili kuepusha taharuki katika jamii na kudumisha amani ikiwemo kukomesha vitendo visivyo vya kiungwana kama ukatili wa kijinsia.