skip to Main Content

MPANDA

Baadhi Ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa maoni mseto juu ya wimbi lililoibuka la watu wanaofanya matukio ya kupora na kuiba mitaani maarufu kama Damu Chafu.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na kituo hiki na kusema kuwa wanahofia sana juu ya usalama wao hasa nyakati za usiku.

Akizungumza katika kipindi cha meza ya busara Inspector Kelvin Fuime kutoka Jeshi la Polisi Kitengo cha dawati la Jinsia na watoto amesema tayari wamekwisha kuwakamata baadhi ya wahalifu pamoja na wazazi wao na kuwa wanaendelea kuwatafuta.

Aidha Inspector Fuime amesema baadhi ya viongozi wanaoongoza makundi hayo wamekamatwa huku akiwataka wahalifu kuachana na matukio hayo.

Back To Top