skip to Main Content

KATAVI
Kijiji cha Kayenze kata ya Katuma Wilayani Tanganyika mkoani Katavi kimepanga kuchangishana kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la Choo katika Soko Linalomilikiwa na kijiji.

Diwani wa kata ya katuma Paulo Pamasi ameiambia mpanda Radio kuwa kuanzia mwezi ujao mara baada ya kukaa Vikao wataanza kuchangishana ili kukamilisha ujenzi wa Vyoo katika soko hilo.

Akizungumzia changamoto hiyo Mwenyekiti wa Kayenze B bwana Vicent Kadogosa amekiri kutokuwapo kwa Choo katika soko lililopo huku akielezea uwepo wa shimo lililochimbwa ambalo litakapokamilika ndiyo kita kuwa chooo cha soko la Kijiji.

AWALI wanachi wa Kijiji hicho wamelalamikia kutokuwapo kwa choo katika soko hilo kutapeleka mlipuko wa magonjwa ambayo yangeweza kuepukika kama kungekuwa na miundombinu mizuri sokoni hapo.

Back To Top