skip to Main Content

KATAVI

Wananchi wa Kayenze kata ya Katuma Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wameiomba serikali kumhimiza mkandarasi anayejenga mradi wa maji kukamilisha mradi kwa wakati.

Wananchi Kwa nyakati Tofauti wameiambia Mpanda radio kuwa kumekuwa na adha kubwa ya upatikanaji wa maji safi kwa matumizi hivyo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko wameiomba Serikali iwasaidie kuondoa hadha hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji B Kayenze Vicent Kadogosa ameiomba serikali kusaidia kuwahimiza Wakandarasi waharakishe ukamilishwaji wa Mradi huo ili wananchi waweze kunufaika.

Akizungumza kwa Njia ya Simu Meneja wa Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira mjini na vijijini [RUWASA] Wilayani Tanganyika Injinia ALKAM Omar Sabuni amesema kuwa Mradi wa Maji Wa Kayenze unatarajiwa kukamilika Kabla ya kuisha kwa bajeti ya Fedha ya 2022/2023.

Back To Top