skip to Main Content

MPANDA

Baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani katavi wametoa maoni mseto ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita Dr Samia Suluh Hassan baada ya kutimiza miaka miwili ya uongozi wake.

Wakizungumza na kituo baadhi ya wananchi hao wametaja baadhi ya mambo ambayo wamenufaika katika uongozi wa rais Samia kuwa ni pamoja na kuendelea kuwapa nafasi wanawake katika nyanja mbalimbali huku pia wakiendelea kuboreshewa mikopo ambayo imekuwa chachu ya mafaniko.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli ametaja baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa chini ya uongozi wa Dr Samia Suluh Hassani huku akiwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais.

Back To Top