skip to Main Content

KATAVI

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani Wananchi wa mkoa wa Katavi wameombwa kujitokeza katika viwanja vya kashaulili kwa ajili ya kupima na kupatiwa matibabu bure.

Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Idary Sumry amesema kuwa wananchi wanapaswa kutumia kipindi hiki kufahamu afya zao huku akiwataka watoa huduma kufanya kazi kwa bidii na kutimiza wajibu wao

Robedi Nguma ni Muuguzi mkuu wa mkoa wa Katavi amesema kuwa huduma zote zinazopatikana ni kama kupima uviko 19,uzazi wa mpango,kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi ambapo huduma zote zinatolewa bila malipo

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliofika katika viwanja hivyo wamepongeza huduma inayotolewa na kuwataka wananchi kufika na kupatiwa huduma.

Maadhimisho ya siku ya wauguzi dunia kwa mkoa huu yameanza tarehe 8 na kilele chake ni tarehe 12 ya mwezi huu yakiwa na kauli mbiu isemayo..wauguzi wetu mstakabali wa Maisha yetu.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayaafya

#TBC

#wasafifm

#cloudsfmtz

Back To Top