Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wakulima wa zao la Pilipili Mikoa ya Katavi na Songwe wametakiwa kutumia fursa ya kujikwamua kiuchumi kwa kujizatiti katika kilimo cha zao la pilipili ambalo kwa sasa soko lake ni la uhakika na lenye fursa.
Akizungumza na Mpanda radio fm Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Mkoa wa Mbeya Nzenga Simbeye amesema katika Mpango mkakati wa kuunda jukwaa la wadau wa pilipili utaowawezesha vijana kunufaika na zao la pili pili na kuwataka vijana kuhamasika na fursa ya zao hilo.
Awali akichangia mmoja ya wadau wa biashara ya viuongo ikiwemo pilipili kichaa Barcho Masooud Amewataka wakulima wa zao la pilipili pamoja na wafanyabiashara wa zao la pilipili kichaa kuongeza juhudi katika uzalishaji wa zao hilo na kuwataka kufanya biashara kwa kungalia soko linahitaji kitu gani.
Wadau wa Jukwaa la pilipili Mkoa wa katavi na Songwe wamekutana pamoja ili kuweka Mpango Mkakati wa kuhakikisha zao hilo linatangazwa Kwa kuanzisha jukwaa la wadau wa pilipili , ambalo kwa sasa limekuwa fursa kubwa kiuchumi.