Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wakulima Kata ya Makanyagio wametakiwa kuendelea kujiandikisha katika maeneo wanayofanyia shughuli za kilimo ili kunufaika na ruzuku ya mbolea iliyotolewa na serikali.
Akitoa ufafanuzi huo wakati akizungumza na Mpanda Radio Fm mtendaji wa kata hiyo Dolnad Edward amesema serikali ilitoa utaratibu wa wakulima wanaoishi maeneo ya mjini kwenda kujiandikisha ruzuku ya mbolea maeneo wanayofanyia shughuli za kilimo ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.
.
Aidha Dolnad amewaomba wakulima kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na wale ambao bado hawajui utaratibu wafike ofisini ili kupewa maelekezo na kunufaika na ruzuku hiyo.
.
Ruzuku ya mbolea ilianza tangu Agosti 15 mwaka huu kwa nchi nzima lengo likiwa ni kuinua sekta ya kilimo nchini.