Afisa ustawi manispaa ya mpanda Anyulumye Longo. Picha na Leah Kamala Na Leah Kamala Baadhi…

Na Samwel Mbugi
Wafanyabiashara wa soko la Mpanda hotel wameiomba serikali kushughulikia changamoto ya mifereji ya kupitishia maji hususani kipindi hiki cha mvua zilizoanza kunyesha ili isije kuleta madhara ya magojwa ya mlipuko.
Wameyasema hayo wakizungumza na Mpanda radio FM kuwa kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha kumejitokeza madhara ya kujaa kwa maji katika soko hilo na kusababisha kukosa wateja wa bidhaa zao ambazo zinakuwa zimeshalowa.
Katibu wa soko la Mpanda hotel Haji Mponda amesema kutokana na changamoto hiyo, kupitia kwa afisa biashara mkoa wa Katavi alifika eneo hilo na kuahidi kulifanyia kazi kwa kwenda kuonana na TARURA ili wafanye marekebisho ya mfereji uliopo upande wa soko hilo.
