Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wafanyabiashara wa soko la Mahindi Kata ya Mpanda Hotel Manispaa Mpanda Mkoani Katavi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu miundombinu ya soko huku baadhi wakiiomba serikali kuwatafutia eneo pana kwa ajili ya shughuli hiyo
Maoni hayo wameyatoa wakati wakizungumza na kituo hiki ambapo imeonekena kuwa na wafanya biashara wengi wanao ingia na kutoka kwa shughuli za kuuza mahindi lakini hakuna miundombinu rafiki ikiwemo choo katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa soko hilo Ruben Richard amesema kuwa suala la soko hilo kutokuwa na choo limeshafikishwa kwa viongozi ambapo ufumbuzi wake bado haujajulikana
Kwaupande wake diwani wa kata ya Mpanda hotel Hamis Msigaro akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani alibainisha kuwa wafanyabiashara wa soko hilo wanapaswa kujengewa choo ili kusaidia kuondoa adha wanazo kutana nazo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri sofia Kumbuli amekiri kuwa eneo hilo linahitajika choo na kuahidi kutafuta namna ya kufanya ili kujenga choo cha muda wakati serikali ikitafuta eneo maalum ili kuhamishia soko hilo .