skip to Main Content

MPANDA

Wazazi na walezi katika mtaa wa Rungwa kata ya Kazima  Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesikitishwa na kitendo cha ukatili wa kingono kilichofanywa na mwalimu wa kituo cha New Light Day Care huku wakitaka achukuliwe hatua za kisheria ili iwe funzo kwa wengine.

Wakizungumza na mpanda Radio fm wazazi hao wamesema kuwa, kitendo hicho ni cha kinyama kwani hawaoni sababu ya mtu kumuingilia mtoto  na kuwaomba  wazazi wengine kuwa makini katika kufanya chaguzi sahihi ya vituo ambavyo watoto wanaweza kupata elimu na malezi bora

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph alipofanya ziara ya kukagua kituo hicho february 27 aliagiza kituo hicho kufungwa na mkurugenzi wa kituo hicho kuendelea kushikiliwa kwa upelelezi zaidi, kufuatia kitendo cha ukatili wa kingono kilichofanywa na mwalimu wa kituo hicho sambamba na kukosa usajili.

Aidha Jamila ameagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na ustawi wa jamii kuhakikisha wanakaa na watoto ili kuwafanyia uchunguzi kama kuna ambao walisha fanyiwa vitendo vya namna hiyo.

Back To Top