skip to Main Content

KATAVI

Watumishi wa Mahakama nchini wametakiwa kutenda haki na kuepuka vitendo vya rushwa ili kuwahudumia wananchi kwa haki,usawa na kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Jaji Kiongozi Mahakama Kuu Tanzania Mustapher Mohamed Siyani wakati akizungumza katika uzinduzi wa mahakama za hakimu mkazi mkoa wa Katavi,Songwe na Lindi yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi mkoani hapa.

Jaji Siyani amesema kuwa huduma za mahakama zinaendelea kuboreshwa nchini ili kurahisisha huduma za kisheria na mahakama kwa wananchi kwa kuendelea kusogeza huduma hizo karibu na kupunguza muda wa kusikiliza mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Jofrey Pinda amesema serikali ipo katika mpango wa kujenga Mahakama Jumuishi ikiwemo mkoa wa Katavi ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.

Mpanda radio imezungumza na wananchi mkoani Katavi ambapo wameeleza kuwa uzinduzi wa Mahakama hiyo utapunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma hiyo mkoani Rukwa.

Zaidi ya wananchi laki saba walikua wakilazimika kusafiri kwa umbali wa Km 230 kufuata huduma ya Mahakama ya Mkoa iliyopo Sumbawanga.

Back To Top