skip to Main Content

KATAVI

Kufuatia changamoto ya magonjwa ya Tumbo na minyoo jamii imetakiwa kuzingatia kanuni za afya ili kuondokana na magonjwa hayo kwa baadhi ya wakazi wa Itenka Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi.

Hayo yamejiri mara baada ya wakazi wa Intenka halmashauri ya Nsimbo kuzungumza na Mpanda Radio Fm na kueleza kuwa kutozingatia kanuni za afya na pia kukosa maji safi na salama kwa baadhi ya maeneo kumekuwa changamoto kwao ya kupata magonjwa hayo katika jamii.

Akizungumzia suala hilo kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Itenka, MUUGUZI Charles Maligita amekiri kuwa wanapokea Wagonjwa wengi wa magonjwa ya matumbo minyoo na UTI.

Amesema kuwa wanaendelea na jitihada za kutoa elimu mashuleni na kwa jamii juu ya changamoto ya magonjwa hayo na kuitaka jamii kuzingatia kanuni za afya na kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.

Back To Top