skip to Main Content

IVUNGWE

Kukosekana kwa maeneo kwa ajili ya Wakulima na Wafugaji Katika kijiji cha Kasokola Manispaa ya Mpanda   Mkoani Katavi imetajwa kuwa ni sababu inayopelekea mgogoro baina ya wakulima na wafugaji.

 Hayo yamebainishwa na  Mwenyekiti wa kijiji Cha Kasokola Carlos  Joackim Malufwa wakati akijibu hoja za wakulima wa Ivungwe ambao mashamba yao yamevamiwa na wafugaji nakusema kuwa katika  Manispaa ya Mpanda bado hakuna maeneo tengefu kwa ajili ya Kilimo na Ufugaji.

INSERT………….. MKITI KASOKOLA

Wakizungumza na Mpanda radio fm wakulima Kutoka Kijiji cha Kasokola kitongoji cha Ivungwe  wamesema wafugaji wamekua wakiharibu mazao  kwa kulisha mifugo mazao yao na  kupelekea familia kukosa chakula.  

INSERT………… WANANCHI KERO NG`OM BE

 Kwa Mujibu wa Mwenyekiti huyo Kutengwa kwa maeneo maalumu kwa ajili ya wakulima kwa shughuli za kilimo na maeneo kwa ajili ya malisho kwa wafugaji kutaleta suluhu ya mgogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Back To Top