Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MLELE
Zaidi ya Bilioni moja zimetumika katika ujenzi wa minara na kituo kidogo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Wilayani Mlele Mkoani Katavi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye wakati akizindua kituo kidogo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kilichopo wilayani Mlele amesema awali usikivu wa redio hiyo haukuwa mzuri hasa maeneo ya pembezoni mwa mji ambapo kwa sasa adhaa hiyo inakwenda kupungua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dk. Ayub Rioba pamoja na Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Justina Mashiba wamesema mradi huo ni moja ya miradi minne ambayo imeshatekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) hasa kwenye maeneo ya pembezoni mwa mji
Waziri Nape amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani hapa ambayo ilianza Januari 9.