skip to Main Content

KATAVI

Kutokuwa na uhuru wa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo,rushwa,na kutokujua sheria zimetajwa kuwa ni changamoto zinazowakabiri wanawake.

Akisoma Risala , Bi. Chiku Peter na kuwawakilisha wanawake katika kusherehekea siku ya wanawake  duniani iliyofanyika Machi 8 mwaka huu amesema kuwa  changemoto mbalimbali zinawakumba wanawake wengi.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa katavi ambae pia ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wanaume kuwaruhusu wenza wao kufanya kazi ili kuleta maendeleo kwenye jamii.

Siku ya wanawake duniani kwa mkoa wa katavi imefanyika katika halmashauri ya Tanganyika  huku ikiambatana na kauli mbiu isemayo ‘Ubunifu na mabadiriko ya teknolojia chanya katika kuleta usawa wa kijinsia’.

Back To Top