miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
MPANDA
Chama cha ACT Wazalendo kimewataka wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kufanya mabadiliko ya kiuongozi ifikapo mwaka 2025 ili kuepukana na changamoto mbalimbali za kimaisha ambazo wamekuwa wakikutana nazo.
Hayo yamezungumzwa na uongozi wa chama cha ACT katika mkutano uliofanyika viwanja vya sikonge Manispaa ya Mpanda.
Mwanahabari wetu Ben Gadau alikuwepo katika Mkutano huo na hapa anatufahamisha kilicho jili viwanja hapo.
KATAVI.
Mwanamke mmoja anaeishi mtaa wa Kigamboni Kata ya shanwe amenusurika kifo baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kugundurika kumtupa mtoto wake. Huyu hapa ANNASTAZIA FILIMBI Ametusogezea undani wa taarifa hiyo.
MPANDA
Wakazi wa mtaa wa kigamboni kata ya shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi.
Wakizungumza na Mpanda Radio fm wananchi hao wamesema kuwa licha ya kata yao kuwa karibu na bwawa na milala ambalo linaweza kuhudumia sehemu kubwa ya mji wa Mpanda, Undani wa taarifa hii tuungane na mwandishi wetu, KINYOGOTO FESTO.
MPANDA
Baadhi ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makanyagio iliyopo Kata ya Shanwe Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa Katavi wameushukuru uongozi wa Mkoa kwa kuwawezesha ujenzi wa madarasa yanayotekelezwa na mradi wa BOOST.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na MWANDISHI WETU LUSY DASHUD alipotembelea shuleni hapo ambapo ujenzi unaendelea.
KATAVI
Mkoa wa Katavi umepiga marufu wafanyabiashara wa mazao wanaotoka nje ya Tanzania kuacha kununua mazao moja kwa moja kwa wakulima.
Tamko hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ambapo amesema kuwa wafanya biashara kutoka nje ya nchi wanapaswa kununua mazao kutoka kwa wafanyabiashara waliopo mkoani hapa huku akiwataka wafanyabiashara wa ndani wananunua mazao kwa mkulima kwa bei Rafiki, kwa undani zaidi wa habari hiyo tuungane na JOHN BENJAMIN.
KATAVI
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa katavi imeongeza huduma katika kitengo cha kutengeneza viungo bandia ambapo hapo awali huduma hiyo ilikuwa haipatikani mkoani hapa.
Miongoni mwa huduma ambazo zimeongoza ni kipimo cha CT SCAN,Huduma ya miwani,huduma ya upasuaji wa aina zote na huduma ya utengemao .Na mwanahabari Wetu GLADNESS RICHARD anatuarifu undani wa taarifa hii.
MPANDA
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa Katavi wameiomba Serikali kufanya ukaguzi wa kina kwenye viwanda vyote vya chakula na vinywaji ili kubaini kasoro zinazo jitokeza katika biadhaa hizo ikiwa ni Pamoja na madawa ya kulevya ambayo yametajwa kuonekana katika baadhi ya bidhaa ikiwemo biskuti na Asali
Veronica Mabwile anaundani wa taarifa zaidi.
MICHEZO
Kambi ya timu ya UMITASHMTA ngazi ya mkoa inaendelea vizuri mkoani hapa, Patrick Rweyemamu amepata nafasi ya kusimamia timu za vijana katika kikosi hicho, na kimataifa leo ni fainali ya Europa Leage.
Mwanamichezo wetu Killian Samwel huyu hap ana taarifa zaidi.