skip to Main Content

KATAVI
Kamishna wa ardhi mkoa wa katavi amemuomba Naibu wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi Geofrey Pinda kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi katika ofisi za ardhi.

Akizungumza Kamishna wa ardhi Geogrey Martin amesema idara ya ardhi imekuwa na uhaba wa watumishi huku akisema kutokana na changamoto hiyo imekuwa ikipelekea baadhi ya shughuli kushindwa kufanyika kwa wakati.

Aidha kamishna ametaja miongoni mwa changamoto zinazokwamisha utendaji nikukosekana kwa usafiri katika idara ya ardhi huku akitaja kama ni miongozi mwa vikwazo katika utendaji wao wa kazi.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo na makazi Geofrey Pinda amewataka watumishi wa idara ya ardhi kufanya kazi wa weredi bila kusababisha migogoro huku akisema changamoto hizo zinatafutiwa ufumbuzi.

Back To Top