skip to Main Content

MPANDA.

Nyumba mbili zimeezuliwa katika mtaa wa mtemi beda kata ya misunkumilo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo na kusababisha watu kukosa makazi .

Wakizungumza na mpanda redio fm wahanga wa tukio hilo wamesema kuwa tukio hilo limetokea wakiwa wamekaa ndani na familia zao wakati mvua ikiendelea kunyesha , upepo mkali ulivuma uliosababisha kuezuka kwa paa na kuharibu vitu vilivyomo ndani ya nyumba hizo

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa mtemi beda Edes Paul Kazwika amekiri kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake huku akisema kuwa katika tukio hilo hakuna watu waliojeruhiwa wala vifo vilivyotekea .

Mvua hiyo imedumu kwa takribani masaa mawili huku ikiambatana na upepo mkali pamoja na radi.

Back To Top