skip to Main Content

KATAVI

Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 14 amekutwa ametupwa kwenye mlango wa nyumba ya Jenifa Donald mkazi wa Tambukareli mtaa wa Shauritanga Manispaa ya Mpanda.

Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza na Mpanda radio wamebainisha kuwa mtoto huyo amekutwa akiwa ametelekezwa mlangoni nyumbani usiku wa kuamkia april 03

Aidha Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Shauritanga Ana Wilson amesema baada ya kupata taarifa aliwasiliana na Mwenyekiti wa Mtaa ambapo wameshauriana kumpeleka mtoto kwe nye kituo cha kulelea watoto kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukareli Celestine Shauritanga amelaani tukio hilo na kusema ni tendo la Kinyama na halikubaliki na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mama mhusika pindi atapobainika.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tambukareli hilo ni tukio la kwanza kutokea mtaani kwake.

Back To Top