Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MLELE
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mlele Wolfgang Mizengo Pinda amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Kwa utekelezaji wa Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kutokana na fedha za Serikali Kuu na usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
Pinda ametoa pongezi katika ziara ya Kamati ya Siasa Wilaya ilipofanya ziara kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama..
Miradi iliyotembelewa ni miradi ya Sekta ya Elimu Msingi,Elimu Sekondari,Miradi ya Sekta ya Afya,Miradi ya Sekta ya Maji Pamoja mradi wa Sekta ya Miundo mbinu ya barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA.
Kamati imekagua barabara ya kutoka Inyonga hadi Nsenkwa inayojengwa kwa kiwango cha lami,na ujenzi wa barabara za mjini katika mji wa Inyonga,na kupokea taarifa ya ujenzi wa barabara hizo.
Kamati vilevile imetembelea ujenzi wa Bwawa la kusambaza maji katika Mji wa Inyonga lililoko Kata ya Nsenkwa bwawa ambalo linajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.9 fedha kutoka Serikali Kuu na Kujionea hali halisi ya Maendeleo ya Mradi huu.