skip to Main Content

TANGANYIKA
Katika kuimarisha huduma za kimahakama mkoani Katavi Serikali imejipanga kujenga majengo mapya katika makao makuu ya tarafa zote wilayani Tanganyika.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa katiba na sheria Geofrey Pinda wakati wa ziara ya waziri Mkuu Kassim Majaliwa Katika Kijiji cha Sibwesa Wilayani Tanganyika na kusema kufikia mwaka 2025 kutajengwa majengo mapya ili kuleta huduma karibu kwa wananchi.

Aidha Geofrey amemwagiza mkurugenzi mkuu wa mashitaka [DPP] kufuatilia kesi za kubambikiziwa ili kuwapa nafasi wananchi wasio na hatia kuachiwa huru.

Katika hatua nyingine Pinda amesema Mkoa wa katavi unatarajia kujengewa mahakama jumuishi ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Back To Top