skip to Main Content

MPANDA
Kutokana na kuendelea kukithiri kwa changamoto ya magari ya shule kubeba wanafunzi idadi kubwa kuliko uwezo, wananchi mkoani Katavi wamewataka wamiliki wa shule kuzingatia sheria zinavowataka.

Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi wamesema kuwa wameshuhudia baadhi ya magari hayo kujaza wanafunzi wengi na kupunguza usalama wa wanafunzi na kuwataka wamiliki kuongeza magari ili kuendana na idadi ya wanafunzi na kuongeza usalama.

Kwa upande wake Askari wa usalama barabarani kutoka ofisi ya afisa wa usalama barabarani mkoa wa katavi John Thomas amewakumbusha madereva kubeba idadi ya watu kutokana na kadi ya gari inavyoonyesha.

Back To Top