Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Uwepo wa Klabu za kutoa elimu mashuleni imetajwa kuwa moja ya sababu ambazo zinamsadia mwanafunzi katika masomo na Maisha yake kwa jamii
Baadhi ya wanafunzi katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema wamekuwa wakipata elimu ya ugonjwa wa ukimwi,namna ya kupambana na rushwa huku wakiwaomba wadau kuwa na ratiba ya kuwatembelea mashuleni.
Mwalimu Peter Limbu makamu mkuu wa shule ya sekondari Mwangaza halmashauri ya manispaa ya Mpanda amesema kuwa elimu ambayo imekuwa wakipatiwa wanafunzi kupitia klabu imekuwa na tija katika masomo hivyo amewaomba wadau kuendelea kuunga mkono klabu hizo ili ziendelee kuwahudumia wanafunzi wa shule mbalimbali.
Kumekuwepo na taratibu za shule kuanzisha klabu za kuwasaidia wanafunzi kupata elimu kutoka kwa wadau wa tasisi za serikali na binafsi.