skip to Main Content

picha na Mtandao

Katavi

Wananchi wa Mtaa wa Mpanda hoteli manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanafanya usafi  kwenye  mazingira yanayowazunguka .

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa mtaa huo Christina Mshani  wakati wa kilele cha  kampeni ya usafi iliyoandaliwa na kikundi cha TRANS CARGO.

Ibrahim Msanda amabaye ni mwenyekiti wa kikundi cha TRANS CARGO amesema usafi umefanyika maeneo mbalimbali lengo likiwa  ni kuhakikisha manispaa inakuwa safi.

Kwa upande wake  mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Haidary Sumry  ambaye alikuwa mgeni  rasmi amesema  kuna baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa hawatoi ushirikiano katika suala la usafi jambo ambalo   halipendezi.

Kilele cha kampeni  hiyo ya  usafi kimefanyika Kata ya Mpanda hotel ambapo kata ya Kashaulili imeongoza kwa usafi huku kata ya  Nsemulwa ikifanya vibaya katika usafi na kupewa kinyago.

Back To Top