skip to Main Content

Katavi

Katibu wa Chama cha demokrasia na maendeleo  Sospeter Chotola Mkoani Katavi  amepokea barua ya kutia nia ya kugombea nafasi ya ubunge  kutoka kwa mwanachama  Masanja Mussa Katambi .

Akizungumza na vyombo  vya habari  katika ofisi za chama mkoa Chotola amesema hatua hiyo ni kufuatia  tangazo la kuwataka wanachama  kutia nia   ya kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi serikalini  ndani ya  chama .

Masanja mussa Katambi ambaye ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la mpanda mjini  amesema amejianda katika Nyanja zote na anaamini akiwa kiongozi atakuwa chachu ya maendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho jimbo la mpanda mjini amempongeza mwanachama huyo na amewakaribisha wanachama wengine  kujitokeza  kutia ya  kuwani nafasi  jimbo  hilo.

Back To Top