miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
KATAVI
Mkoa wa katavi umezalisha kilogramu za pamba milioni mbili laki moja na sabini na tatu elfu mia tatu tisini na tisa katika msimu wa mwaka 2020/2021 ikiwa ni chini ya kiwango kinachohitajika katika soko la pamba.
Kauli imetolewa na katibu tawala wa mkoa wa katavi Rodrick Mpogoro kwenye kikao cha uhamasishaji wa zao la pamba mkoani hapa na kusema mkoa wa katavi umezalisha kiwango kidogo cha pamba katika msimu wa mwaka 2020/2021 licha ya kuwepo kwa soko la pamba la uhakika.
Kwa upande wake mwakilishi wa bodi ya pamba Renatus Luneja ambae ameambatana na balozi wa pamba Tanzania amesema mkoa wa katavi ni moja ya mikoa ya kimkakati katika uzalishaji wa zao la pamba ameongeza kwa kusema licha ya kuzalisha mbegu za zao hilo, mkoa unatakiwa kuzalisha tani elfu hamsini za pamba katika msimu wa 2021/2022.
Kampeni ya kuongeza tija na uzalishaji wa zao la pamba ilizinduliwa rasmi tarehe 4 mwezi july mwaka huu katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.