“Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wananchi wilayani humo kuacha kujihusisha na na…
MPANDA
Mkoa wa Katavi umefikia zaidi ya asilimia 70 katika usambazaji wa maji safi na salama vijijini, huku lengo kuu ikiwa ni kutatua changamoto hiyo katika vijiji vilivyosalia.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mitambo ya uchimbaji wa visima vya maji kupitia fedha za uviko ambapo amewaaasa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini na mjini [Ruwasa] kuhakikisha wanavitumia vifaa hivyo katika kuendelea kutatua changamotoya maji.
Akipokea vifaa hivyo meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini na mjini [Ruwasa] Mkoa wa Katavi Injinia Peter Ngunula ameishukuru serikali ya awamu ya sita na amesema watavitumia vifaa hivyo kuhakikisha wanafikia zaidi ya asilimia 80 mwaka 2025 huku kipaumbele kikiwa ni zile sehemu zenye changamoto zaidi hasa katika maeneo ya vijijini lengo ikiwa ni kumtua mama ndoo kichwani.
Katika hatua nyingine Mrindoko amesema kwa kipindi cha miaka miwili Mkoa wa Katavi umepokea zaidi ya shilingi bilioni 25 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ambayo miradi 17 imekamilika na miradi 25 ikiwa katika hatua za muendelezo.