skip to Main Content
This image has an empty alt attribute; its file name is godogo-1024x683.jpg

Diwani wa kata ya sitalike halmashauri ya Nsimbo( anayepeana mkono na mwanafunzi)na viongozi wengine wakiwa katika maadhimisho hayo wakigawa magodoro kwa wanafunzi.

Na Lilian Vicent -Katavi

Kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ambayo hufanyika kila  tarehe 16 mwezi wa sita kila mwaka  , halmashauri ya wilaya ya Nsimbo imefanya maadhimisho hayo katika kijiji cha Mtisi ,kitongoji cha Magula kata ya Sitalike ambapo wazazi wametakiwa  kuacha kuwaozesha watoto wa kike wakiwa na  umri mdogo badala yake  wawaache wasome

Hayo yamesemwa na diwani wa kata hiyo ya Sitalike Adam Chalamila wakati akiwahutubia wananchi hao na ameongeza kuwa mara nyingi wanapopokea kesi za wanafunzi waliopewa mimba zimekuwa zikiisha kwa makubaliano baina ya wazazi na watuhumiwa jambo ambalo halipaswi kufanyika hivyo .

 Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii  wa halmashauri hiyo Theresia Mwendapole  amesema wameamua kufanya maadhimisho hayo  eneo hilo kutokana na kuwa na  changamoto za mimba za utotoni na ndoa za utotoni.

Nao baadhi ya wananchi wamesema ni kweli wazazi wamekuwa wakiwaozesha watoto wadogo na wengine wamekuwa wakiacha chuo na kutumikishwa kama wafanyakazi na wazazi wao.

Kauli mbiu katika maadhimisho ya mtoto wa Afrika inasema ‘elimu jumuishi kwa watoto izingatie  maarifa ,maadili na stadi za kazi’’

Back To Top