skip to Main Content

miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na Samwel Mbugi

Katavi

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda wamezitaka mamlaka kutatua changamoto  ya mrundikano wa uchafu katika makazi.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM  ambapo wamesema  taka hizo zimekuwa kero kutokana na kukaa bila kuzolewa licha ya kutoa pesa   za kutoa takataka hizo katika makazi yao

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco Ivo Chambala amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo inasababishwa na uchache wa magari ya kubeba taka pamoja na ubovu wa miundombinu ya Barabara kuwa ni moja ya sababu zinazosababisha mrundikano mkubwa wa takataka.

Hata hivyo jitihada zinaendelea kufanyika ili kuwapata wenye mamlaka husika ambao wanaweza kutolea ufafanuzi  dhidi ya changamoto hizo

Sambamba na hilo   mwenyekiti Chambala amewataka Wananchi wa mtaa wa Mpadeco kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la wakazi litakalotumika November 27 mwaka huu kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.

Back To Top