skip to Main Content

Daraja ambalo Wajumbe wa kamati ya siasa hawajaridhishwa nalo kutokana na mkandarasi kutofuata maagizo.

hawajaridhishwa na mkandarasi wa ujenzi wa daraja la tulieni kwani hajafuata maagizo ya chama ya  kufanya marekebisho.

Liliani Vicent -Katavi

Wajumbe wa kamati ya siasa  chama cha mapinduzi CCM Kata ya Nsemulwa  manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema hawajaridhishwa na mkandarasi wa ujenzi wa daraja la tulieni kwani hajafuata maagizo ya chama ya  kufanya marekebisho.

Wameyasema hayo  wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali  ya maendeleo katika kata hiyo ambapo   mkandarasi ametakiwa kurudi kujenga kwa kiwango kinachotakiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa kata  hiyo Alex Ngereza amesema   mkandarasi  alipewa maelekezo ya kufanya marekebisho lakini hajafanya hivyo ambapo hatua zitachukuliwa kwa manufaa ya wananchi.

Ziara ya  ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Kata ya nsemulwa   ilianza tarehe 23 mwezi Agost ambapo wametembelea shule ya msingi tulieni na kilimani ,kituo cha afya ,daraja la tulieni na umaliziaji  wa wodi za kinamama.

Back To Top