skip to Main Content

KATAVI
Jumla ya kesi 35 za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto mkoani Katavi zimesikilizwa na kutolewa hukumu mahakamani katika kipindi cha mwezi Januari mbaka Novemba 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad amesema katika mafanikio ya kesi hizo kumekuwa na ongezeko la kesi 8 sawa na asilimia 29.6 ukilinganisha na mwaka 2021 ambapo jumla ya kesi 27 zilisikilizwa na kutolewa maamuzi.

Katika hatua nyingine Makame amesema kumetokea tukio la unyanganyi wa kutumia nguvu ambapo mnamo tarehe 30-11-2022 katika kijiji cha Mtisi kata ya Sitalike Wilaya ya Mpanda familia ya Moses Edward Kalambo imevamiwa na kundi la watu sita na kuvunja mlango kuiba vitu vya ndani

Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi linatoa wito kwa wananchi wanaojihusisha na matukio ya kihalifu kuacha mara moja na badala yake wajikite katika kufanya shughuli zao halali.

Back To Top