skip to Main Content

KATAVI.

Jamii ya mkoa wa katavi imeshauriwa kuwaandaa vijana kuanzia ngazi ya msingi kuwapa uwezo wa kuwa viongozi bora.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo cha afya shirikishi manispaa ya mpanda Lightness Michael  na kusema kuwa kila mwananchi anaowajibu wa kumuandaa kijana kujiamini na kuwa kiongozi bora katika jamii kwani kwa kufanya hiyo kutakua na viongozi wazalendo na wenye uchungu na taifa lao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani hapa wamekua na maoni tofauti juu ya kumuandaa kijana kuwa kiongozi kuanzia ngazi ya msingi na kusema kuwa ili kupata viongozi bora ni lazima jamii iwajibike.

Ripoti ya umoja wa mataifa imesema kwamba vijana bilioni 1.2 kote ulimwenguni wenye umri kati ya miaka 15-24 ni muhimu kuwaandaa kuwa viongozi bora katika kufanikisha jamii endelevu

.

Back To Top