skip to Main Content

MPANDA

Diwani wa Kata ya Uwanja wa Ndege Mkoani Katavi Kamande Mbogo ametoa usafiri wa baiskeli kwa makatibu wa tawi wa Chama Cha Mapinduzi Kata ili kuwarahisishia shughuli za utendaji wanavotekeleza ilani ya chama.

Akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wananchama amesema ameona upo umuhimu wa makatibu hao kupata usafiri, ili kufanya shughuliza chama kwa urahisi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi katika Kata ya Uwanja wa Ndege amewataka makatibu waliopewa usafiri huo kuutumia katika kufanya shuguli za chama kutokana na jiografia ya kata ilikuwa vigumu kuwafikia wananchama wote.

Kwa upande wa makatibu waliokabidhiwa baiskeli wamesema kuwa watazitumia katika shuguli za chama kwani hapo awali walikuwa wanapata changamoto kuwafikia baadhi ya wanachama ilikuwa vigumu kukamilisha shughuli za chama.

Back To Top