skip to Main Content

KATAVI

Jumuiya ya Wazazi mkoani Katavi kupitia chama cha Mapinduzi [CCM] imeleza kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vinavyo endelea kujitokeza vinachangiwa na utumikishaji wa watoto katika shughuli za ujasiliamari pamoja na utelekezaji wa familia .

Hayo yamebainishwa na katibu wa jumuiya ya wanawake mkoa wa Katavi Jenifer Chinguile kwa niaba ya katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa Bashiru Kambarage wakati akizungumza na kituo hiki ofisini kwake na kusema ukatili unaozungumziwa kwa sasa unaanzia kwenye familia kutokana na wazazi au walezi kushindwa kutimiza majukumu ikiwemo kuwahudumia watoto

Kwaupande wa wazazi mkoani Hapa wamesema kuwa ili vitendo viweze kudhibitiwa katika jamii ni muhimu kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji taarifa kwa jeshi la polisi ili kusaidia washukiwa wamatukio ya ukatili kuchukuliwa hatua

Miongoni mwa madhara ya vitendo vya ukatili kwa watoto ni Pamoja mimba za utotoni ,mtoto kuathirika kisaikolojia ,vifo,

Pamoja na migogoro katika jamii

#mpandaradiofm97.0

#ccm

Back To Top