skip to Main Content

NSIMBO

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi kupitia Kwa Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Girbert Samnpa ametoa Wito kwa Jumuiya ya wa wazazi ya Chama hicho kuungana na serikali katika kukemea Mmomonyoko wa Maadili katika Jamii.

Ametoa wito huo wakati akifungua maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya Umoja wa wawazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Itenka Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.

Samnpa amesema kuwa Jumuiya hiyo ya umoja wa wazazi inao wajibu wa kukemea vitendo vya Mmomonyoko wa Maadili kwa kuwa Jumuiya hiyo ndiyo Mlezi wa Viongozi katika kusimamia Maadili kwa viongozi wa Jumuiya ndani ya Chama hicho.

Katika hatua nyingine amesema Jumuiya ya wazazi imekuwa mlezi na imejihusisha katika Malezi na Elimu kwa Vitendo zaidi ndani ya chama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya Wazazi Mkoa wa Katavi Evarist Mnyere amesema Majukumu ya Jumuiya ni Kusimamia Mazingira, Malezi na Elimu.

Uzinduzi wa Wiki ya Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika mkoa wa Katavi imeenda sambamba na Upandaji wa miti katika Kiwanja Kinachomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Itenka,Kufanya Matendo ya Huruma kwa kuwajulia hali wagojwa katika Kituo cha Afya Itenka pamoja na kupanda miti kwenye Kituo hicho.

#mpandaradiofm97.0

#manispaayampanda

#ccm

#TBC

#cloudsfmtz

#wasafifm

Back To Top