skip to Main Content

KATAVI
Wananchi mkoani Katavi wameeleza namna wanavyo mkumbuka aliyekuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli,na kueleza pia jitihada zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita Dk Samia suluhu Hassain .

Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamesema kuwa licha ya Mambo makubwa aliyoyafanywa na Hayati Magufuli kipindi cha uhai wake, wamempongeza rais Samia kwa kuyabeba maono na kuyaendeleza kwa namna ya kipekee.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi Idd Kimanta amesema kuwa chama cha mapinduzi ( CCM ) kimebeba maono aliyokuwanayo hayati magufuli, na kupitia Rais Samia chama hicho kitaendelea kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanapata maendeleo yanayostahili.

March 17, 2021 nchi ya Tanzania ilimpoteza aliyekuwa Rais wa awamu ya tano akiwa madarakani, na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa makamu wa rais kwa mujibu wa katiba, ambapo historia imeandikwa ya mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini Tanzania.

Back To Top