skip to Main Content

DAR ES SALAAM.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kuanzia Jumatano Mei 3, 2023 huku bei ya mafuta ya petrol na dizeli zikipaa.

Taarifa Ambayo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Dk James Mwainyekule imeonyesha kwa mafuta yanayoingia kupitia bandari ya Dar es Salaam bei ya petroli itauzwa 2,871 mwezi huu ikilinganishwa na Sh2,781 ya Aprii.

Hali kadhalika, bei ya dizeli imeongezeka kidogo kutoka Sh2,847 Aprili hadi Sh2,871 mwezi huu sawa na ongezeko la Sh24.

Aidha taarifa imebainisha utofauti katika mikoa ya kaskazini ikijumuisha Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambao bei za mafuta ya petrol na dizeli zitasalia kama ilivyokuwa Aprili Sh2,756 na Sh2,900 mtawalia huku Utofauti wa bei katika mikoa inasababishwa na umbali wa usafirishaji wa mafuta kutoka bandarini na bandari ambayo mkoa husika unachukua mafuta hayo.

Kwa upande wa mafuta yanayoingia kupitia bandari ya Mtwara ambayo inahusisha mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma) bei ya mafuta ya petroli na dizeli ya rejareja itabaki kama ilivyokuwa Aprili kwasababu hakuna shehena mpya ya mafuta iliyopokelewa.

Huku mkoani Katavi Bei za petrol na diesel zikisomeka shilingi 3029 kwa baadhi ya vituo vya kuuzia mafuta ikiwa ni siku ya kwanza kwa bei mpya kuanza kutumika kwa mwezi huu wa tano.

#mpandaradiofm97.0

#ewura

#wizarayanishati

Back To Top